Quantcast
Channel: Human Rights – Vijana FM
Viewing all articles
Browse latest Browse all 14

Ufe-dhuli

$
0
0

Nani muhalifu, aliyeiba kuku akauwawa, au aliyeibiwa kuku alafu akafanya mauaji?

Picha kwa hisani ya blog ya Akida; via wavuti.com

Mara nyingi tukiona hizi picha za kutisha tunaona muhalifu ameshahukumiwa kikatili, huku pembeni yake kukiwa na wananchi wanaoshangalia mwili wake uliolowa damu au uliogeuka mkaa.

Je, wanapiga picha wanaweza kusaidia kupambana dhidi ya huu ufedhuli, kwa kubadilisha angle ya kamera zao? Labda inabidi tuanze kuonesha matukio haya tofauti kidogo, ili kubadilisha mitazamo yetu juu ya unyama huu.

Nadhani kamera zingeanza kuelekezwa sio tu kwa mhalifu anayefanyiwa unyama, bali pia kwa wale ambao wanafanya unyama huo. Kwa mfano, kamera inaweza kuelekezwa kwa mtu mmoja anayenyanyua tofali au jiwe la kumpondea muhalifu kichwani. Inabidi tuanze kuwafahamu hawa mafedhuli mmoja mmoja, kwani wengi wao wamekuwa wakijificha ndani ya haya magenge yanayoitwa: “wananchi wenye hasira kali”.

Mpango ni kukusanya ushahidi wa picha za wananchi hao wakifanya mauaji. Nadhani picha za sura zao zikianza kuoneshwa labda tutaanza kufikiria mara mbili. Labda tutaanza kuona aibu, na kuanza kutafuta njia mbadala za kukabiliana na wahalifu wanaorudi uraiani bila kuadhibiwa na sheria. Labda tukijiona sisi wenyewe tukitenda maovu tutaanza kusahihisha mapungufu yetu badala ya kuhukumu ya wengine. Labda, labda, labda…

Mwisho wa yote, ufedhuli huu unasikitisha, unakera na unatutia aibu katika jamii ya Watanzania. Sasa, kama ambavyo majina ya mafisadi yanavyowekwa hadharani na watu wanajiuzulu — ilihali wachache — kwanini tusitumie njia inayofanana, mathalani kutumia picha, kukabiliana na hawa wauwaji?

Ewe kijana, kwanini mimi na wewe tunaendelea kuuana wenyewe kwa wenyewe?


Viewing all articles
Browse latest Browse all 14

Trending Articles